News

UZINDUZI WA UJENZI WA BARABARA YA MPEMBA - ISONGOLE (TZ/MALAWI BORDER KM 50.3) KWA KIWANGO CHA LAMI.

Posted On: Monday 07, October 2019

*Jiwe la Msingi la barabara hii limewekwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, tarehe 05/10/2019.

*Barabara ya Mpemba – Isongole ni barabara kuu inayounganisha nchi yetu na nchi ya Malawi katika Wilaya ya Ileje katika Mkoa wa Songwe kwa upande wa Tanzania na Wilaya ya Chitipa upande wa Malawi.

*Mradi ulianza mwezi August 2017 na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2020 na utagharimu zaidi ya kiasi cha shilingi bilioni 109 na zote ikiwa ni fedha za Serikali kwa asilimia 100%.

*Ujenzi wa barabara hii ni muhimu sana kwani utafungua fursa nyingi za kiuchumi na kijamii, ikiwa ni pamoja na:-


(i) Kurahisisha usafiri na usafirishaji wa watu na bidhaa kwa Mkoa wa Songwe na mikoa ya jirani;


(ii) Kukuza na kuchochea uzalishaji katika sekta za kilimo, madini, viwanda; na


(iii) Kuimarisha ushirikiano na kuhamasisha biashara ndani ya nchi na nchi jirani ya Malawi.


*Hivyo, barabara hii itakapokamilika itakuwa kichocheo kikubwa cha uchumi na ustawi wa jamii katika Wilaya hizi na Taifa kwa ujumla.

*Ujenzi wa barabara hii utahusisha pia ujenzi wa madaraja 4 ambayo ni Katendo (23m), Songwe (20m), Ndembo (18m), Songwe Border (20m) na makalavati makubwa (Box Culverts) 15 na makalavati madogo 147.

*Mkandarasi wa mradi - China Geo Engineering Corportation na
Mshauri Elekezi - Tanroads Engineering Consulting Unit (TECU).