News

SERIKALI KUTUMIA SHILINGI BILIONI 89 KUJENGA MELI MPYA ZIWA VICTORIA

Posted On: Friday 18, October 2019

Serikali kutumia sh bilioni 89 kujenga meli kubwa mpya katika ziwa Victoria mkoani Mwanza yenye uwezo wa kubeba abiria takribani 1200 pamoja, mizigo tani 400 na Magari 20.

Ujenzi wa meli hiyo umeanza mapema mwezi huu hapa nchini pembezoni mwa ziwa Victoria baada ya kumalizika kwa hatua za awali za design na ukataji vyuma ambao ulifanyika nchini Korea katika mji wa Busan ujenzi huu kwa ujumla unatarajiwa kuchukua miezi 24 hadi ukamilika kwake ambapo kwa sasa ujenzi umefikia asilimia 30.

Akizungumza na waandishi wa habari afisa mtendaji mkuu wa huduma za meli(MSCL) Eric Hamissi,alisema kuwa mpaka sasa baadhi ya vifaa vya ujenzi wa meli hiyo vimeshafika katika eneo la kazi na kwa ujumla makointena makubwa 300 yanatarajiwa kuwasili jijini Mwanza hadi mradi huu utakapokamilika.

Naye mwakilishi wa kampuni ya Gas Entec co.Ltd Kutoka Korea ya Kusini Rayton Kwembe alisema kuwa kutokana na uzoefu wa kampuni hiyo katika kujenga meli anauhakika watajenga kwa kufutana na maelekezo ya mkataba na itakamilika kwa wakati ili iweze kutoa huduma kwa wakazi wa ziwa Victoria na watanzania kwa ujumla.

Mwenyekiti wa Timu ya Ufundi ya Mamlaka ya huduma ya Meli ya (MSCL) Eng.Paul Olekashe kwa upande wake ameihakikishia kampuni ya Gas Entec kupata ushirikiano mkubwa kutoka kwa wahandisi na watalaam wengine katika kukamilisha kazi hiyo kwa wakati,kwani watanzania wanaisubilia meli hiyo kwa ham kubwa.

Kwa upande wa mhandisi Thomasi Ngulika kutoka Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Sekta ya Uchukuzi ametoa wito kwa mkandarasi huyo kufanya kazi usiku na mchana na yenye ubora ili kukamilisha kazi kwa wakati na kutoa mafunzo kwa vijana wanaofanya kazi katika kampuni hiyo ili waweze kujifunza na kupata elimu ya ufundi wa meli kutoka kwa wakorea hao.

Mpoyo Genja na Martini Hauka ni vijana waliopata ajira katika ujenzi wa meli hiyo wamesema kuwa uwepo wa ajira hiyo itawasidia kupata fedha ya kujikimu pamoja na elimu ya mambo mbalimbali ya kiufundi kutoka kwa wakorea.

Pamoja na Serikali kujenga meli hiyo pia inafanya ukarabati mkubwa wa meli MV. Victoria, MV. Butiama na ujenzi wa Chelezo yenye uwezo wa kubeba tan elfu nne.