News

SERIKALI IMETENGA FEDHA KUKAMILISHA UJENZI TERMINAL III

Posted On: Tuesday 24, January 2017

Serikali imesema itatoa fedha kwa ajili ya kukamilisha sehemu ya pili ya mradi wa ujenzi waJengo la Abiria la Tatu la abiria (Terminal III) katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam ili kuboresha huduma za usafiri wa anga nchini.

Akizungumza mara baada ya kukagua mradi huo Waziri Prof. Makame Mbarawa amesema ujenzi wa mradi huo sehemu ya kwanza ilifadhiliwa na Benki ya HSBC ya Uingereza hivyo sehemu ya pili Serikali itatoa fedhaili kukamilisha mradi huo.

ā€¯Awamu ya kwanza ya ujenzi huu tulipata mkopo lakini awamu ya pili ya mradi Serikali tumesema hatutachukua mkopo, tutajenga kwa fedha zetu za ndani sababu tuna uzoefu mkubwa wa utekezaji wa miradi kwa kutumia fedha za zetu za ndani'' amesema Prof. Mbarawa.

Aidha, Prof. Mbarawa ameongeza kuwa imarishaji wa viwanja vya ndege nchini unakwendasabamba na uimarishaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) ambao mpaka sasa tayari lina ndege mbili aina ya Bombadier Q400.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Salim Msangi , amesema mpaka mwishoni mwa mwanzoni wa Mwaka huu mradi huo umekamilika kwa asilimia 66 na kazi zinazoendelea kwa sasa ni kuezeka na kumalizia kazi za ndani ya jengo ikiwemo usimikaji wa mitambo ya umeme, viyoyozi na utandikaji wa nyaya na mbomba kwa ajili ya miundombinu ya ndani.

Ameongeza kuwa kazi za nje ya jengo zinazohusishamaegesho ya ndege yamekamilika kwa asilimia 53, maegesho ya magari asilimia 36 naeneo la mitambo na umeme asilimia 46.

Bw. Msangi amesema kuwa mpaka kufikia mwaka 2020 idadi ya abiria wanaotumia kiwanja cha JNIA watafikia milioni 5 kwa mwaka na makadirio ifikapo mwaka 2025 idadi itaongezeka watafiia milioni 5 kwa mwakaa.

Mradi huu wa jengo la mita za mradi za mraba sitini elfu unatarajiwa kukamilikak mwezi Desemba Mwaka huu na utahudumia abiria zaidi ya milioni 6 kwa mwaka na litaweza kuhuduumia abiria 2,700 kwa saa na litakuwa na uwezo wakuhudumia ndege kubwa aina ya Airbus A380.