News

MRADI WA UJENZI WA DARAJA LA KIGONGO-BUSISI (KM 3.2) NA BARABARA UNGANISHI (KM 1.66), MWANZA.

Posted On: Monday 09, December 2019

》Daraja la Kigongo – Busisi ni sehemu ya Barabara Kuu ya Usagara – Geita – Buzirayombo hadi Kyamyorwa inayounganisha Jiji la Mwanza na Mikoa ya Kanda ya Ziwa ya Geita, Shinyanga, Kigoma na Kagera.


》Aidha, sehemu ya Kigongo – Busisi katika Ukanda wa Ziwa Victoria inaunganisha nchi yetu na nchi jirani za Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.


》Mpaka sasa barabara hii inaunganishwa kwa kutumia vivuko vikubwa vitatu vya MV Mwanza, MV Misungwi na MV Sengerema ambavyo vinabeba idadi ya magari takriban 1,600 kwa siku na kutumia zaidi ya masaa mawili na nusu kuvuka.


》Lengo la ujenzi wa Daraja la Kigongo - Busisi ni kuwaondolea wananchi kero za usafiri kati ya Kigongo na Busisi.


》Kuimarisha ushirikiano wa kibiashara ndani na nje ya nchi hususan nchi za Uganda, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

》Pia kuimarisha usalama kwa wasafiri na mizigo ikizingatiwa kuwepo matukio ya meli kuzama katika Ziwa Victoria.


》Ujenzi wa Daraja hili ni sehemu ya juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano katika kukuza shughuli za kiuchumi na za kijamii ambapo litarahisisha usafiri na usafirishaji wa abiria na mizigo mbalimbali na hivyo kujenga Tanzania ya viwanda na kuifanya nchi kufikia uchumi wa kati.


》Ujenzi wa Daraja hilo limesanifiwa kujengwa kwa kutumia teknolojia ya ujenzi wa madaraja marefu (Long Span Bridges), yaani “Extra Dosed Bridge”.


》Aidha, Daraja la Kigongo Busisi lenye urefu wa kilomita 3.2 ni Daraja refu kuliko yote Afrika Mashariki na ni la Sita (6) katika bara la Afrika.


》 Mradi huu unagharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia 100 kwa gharama ya Shilingi Bilioni
700 ikiwemo na fedha za fidia kwa wananchi waliopisha mradi huo.