News

KATIBU MKUU NYAMHANGA AKAGUA DARAJA LA KAVUUU

Posted On: Friday 30, November 2018

Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga, amekagua daraja la kavuu lililokamilika kujengwa katika barabara ya Majimoto-Inyonga yenye urefu wa KM 130.

Katibu Mkuuamesema kuwa lengo la ujenziwa daraja hilo ni kupunguza gharama za usafiri na usafirishaji kwa mkoa wa Katavi.

Daraja hilo lenye urefu wa mita 85.344 limegharamiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa asilimia 100 kwa gharama ya kiasi cha shilingi bilioni 2.718

Mhandisi Nyamhanga ameongeza kuwa kwa sasa daraja hilo limeanza kutumika kwa magari yasiozidi tani 30 na hivyo kufanyakupunguza urefu wa KM 135 endapo mwanachi hatapitia Mpanda.

"Nimeridhishwa kwa kukamilika kwa daraja hili kwani ilikuwa ni kero kwa wananchi wa wilaya hizi kuzunguka umbali mrefu na gharama za usafiri kupanda", amesema Mhandisi Nyamhanga.

Aidha, amewataka Wakala wa Barabara (TANROADS) kuendelea kuifanyia matengenezo barabara hiyo kwa kiwango cha changarawe ambacho itarahisisha kupitika kwa wakati wote.

Naye Kaimu Meneja wa TANROADS mkoa wa Katavi Mhandisi Martin Mwakabende, amemueleza Katibu huyo kuwa kazi za uwekaji wa kitandacha chuma katika daraja hilo ulifanywa pamoja na wahandisi wa ndani ikiwa ni lengo la kuongeza uwezo na uelewa katika ujenzi wa madaraja yanayotumika hasa nyakati zadharura.

Katibu Mkuu wa Sekta ya Ujenzi, Mhandisi Nyamhanga, yupo katika ziara ya kikazi mkoani Kataviikiwa ni lengo la kukagua miradi mbalimbali inayosimamiwa na sekta yake hususani barabara, madaraja na kiwanja cha ndege.